Loading...
HomeMy WebLinkAboutinformational disclosure 4-19_Swahili Fomu ya Ufumbuzi na Uthibitishaji wa Taarifa (ilikaguliwa tarehe 18/10) Jiji la Iowa, 410 E. Mtaa wa Washington, Jiji la Iowa, IA 52240 Piga simu kwa Huduma ya Nyumba na Ukaguzi ikiwa una maswali kupitia nambari 319-356-5130 www.icgov.org/housing Kumbuka: Taarifa zote lazima ziingizwe kwenye fomu. Maingizo ya “Tazama Ukodishaji” hayakubaliki. 1. anwani ya Kitengo: _________________________________________________ 2. Tovuti ya Jiji. Tovuti ya Jiji la Iowa ni www.icgov.org na inatoa taarifa nyingi kuhusiana na Jiji la Iowa na huduma zake. Ili kupata taarifa kuhusu Idara ya Huduma za Nyumba na Ukaguzi, ikijumuisha Idara ya Ukaguzi wa Nyumba za Kukodi, tembelea www.icgov.org/housing. Ili kupata Kanuni za Jiji, tembelea www.icgov.org/CityKanuni. 3. Ukaaji. Idadi ya wakaaji/wapangaji inategemeana idadi ya sehemu za kuegesha za ndani na ukubwa wa ghorofa ya chini. Tafadhali wasiliana na Mkaguzi Mkuu wa Nyumba kupitia 319-356-5135 kwa taarifa zaidi juu ya kiwango cha juu cha makazi kwa nyumba hii. Mtu aliyetia saini hapa chini anathibitisha kwamba wanahusika kufuata sheria ya kiwango cha juu zaidi cha ukaaji unaoshauriwa na Sheria za Jiji na kwamba ukiukaji wa kiwango cha juu cha ukaaji unaweza kupelekea kupigwa faini kwa mmiliki, msimamizi, na/au mpangaji. Hakuna chochote katika nyaraka hii kinamzuia mmiliki au msimamizi kuweka kikomo cha idadi ya wapangaji kwenye nyumba ya makazi chini ya kiwango cha juu kinachoruhusiwa na Sheria ya Jiji. 4. Wapangaji. Majina ya wapangaji, ikijumuisha wale walio chini ya umri wa miaka 18, wanaoweza kuishi kwenye nyumba hii: Jina la Mpangaji Jina la Mpangaji ______________________________________ ______________________________________ ______________________________________ ______________________________________ ______________________________________ ______________________________________ 5. Vyumba vya Kulala. Vyumba vya chini, juu, na vyumba vingine haviwezi kutumiwa kama vyumba vya kulala kama havikidhi mahitaji ya madirisha, sehemu za kutokea, futi za mraba, na masharti mengine ya Sheria za Makazi. Chumba cha chini ni: ______ Kinakalika _______ Hakikaliki Chumba cha juu ni: ______ Kinakalika _______ Hakikaliki 6. Uchafu/Uchakataji Taka. Jaza sehemu hiiikiwa tu nyumba in ina vyumba visivyozidi vinne (4) vya kukaa. Ukusanyaji wa uchafu, taka-chakata, na bidhaa zinazooza kwa nyumba hii ni ____________________ (siku ya wiki). Makontena yanayosambazwa na Jiji au makontena yaliyothibitishwa yatatumiwa kwa uchafu, taka-chakata, na bidhaa zinazooza. Sehemu ya 16-3H-8A-6 ya Sheria ya Jiji inasema kwamba vyombo vya kukusanyia viwekwe kwenye vituo vya kukusanyia baada ya saa tisa mchana siku moja kabla ya kuchukuliwa na lazima yarudishwe kwenye eneo la kuhifadhia siku kama hiyo ya ukusanyaji. Makontena yanapaswa kuhifadhiwa (yanapokuwa hayako kwenye vituo vya kukusanyia) kwenye maeneo yake ya kuhifadhiwa. Uchafu zaidi au vitu vikubwa vunaweza kuchukuliwa kwa tozo ya nyongeza; wasiliana kupitia 319-356-5151 kwa taarifa zaidi. Taarifa zaidi zinapatikana mtandaoni kwenye www.icgov.org/solidwaste au kwa kupiga simu 319-356-5151. 7. Kuegesha. Tunatambua kwamba hatuwezi kuegesha kwenye nyasi au kwenye sehemu za kutembelea za umma na Mpangishaji anatoa _________ sehemu zisizo mtaani zilizotengenezwa au maeneo mengine ya kupaki kama yalivyothibitishwa na Jiji. 8. Kelele/Nyumba isiyo na utulivu. Ni mfarakano mdogo (adhabu yake ni faini ya $65, mpaka $625 pamoja na gharama zingine na gharama za mahakama) kudhibiti "nyumba isiyo na utulivu." Chini ya Shejia ya Jiji katika Jiji la Iowa sehemu ya 8-5-5, "nyumba isiyo na utulivu" ni: Hakuna mtu ataruhusu au kuruhusu kuendelea, bila kuchukua hatua za kisheria kuzuia kitu hicho, mfarakano wowote, ugomvi, kukosa utulivu, au kosa au hali yoyote ambayo inahatarisha kujeruhi mtu au uharibifu, au kelele kubwa, za juu, zisizokubalika zinazoleta kero kwa majiraji, au zinazoleta kero kwa umma , kwenye makazi yanayomilikiwa na mtu au yaliyo chini ya umiliki wa mtu. Kwa madhumuni ya Sehemu hii, "kwa kero kwa umma" inajumuisha kero kwa watu walio mbali zaidi ya makazi husika na/au kupelekea kero kwa mtu kwenye maeneo ya umma, ikijumuisha maofisa wa amani. 9. Theluji na Nyasi. Sheria ya Jiji sehemu ya 16-1A-8A inatoa maelekezo kwamba theluji inapaswa kuondolewa ndani ya masaa 24 kwa inchi 1 ya theluji kushuka na sehemu ya 6-3-2 inatoa maelekezo kwamba nyasi/magugu hayapaswi kuvuka inchi 10 za kimo. Kulingana na upangaji, tunatambua kwamba Mpangaji/Mpangishaji (kata chaguo moja) anahusika kuondoa theluji na Mpangaji/Mpangishaji (kama chaguo moja) anahusika kufyeka nyasi. Mbali na makubaliano kati ya mpangaji na mpangishaji, Sheria ya Jiji inatoa maelekezo kwamba Jiji linaweza kumuwajibisha mmiliki, msimamizi au mpangaji, na ukiukaji wa sehemu yoyote iliyonakiliwa hapo juu unaweza kupelekea kupigwa faini ya $250.00 kwa ukiukaji wa kwanza na/au Jiji kufyeka nyasi/kuzoa theluji na kukadiria gharama ya kazi hiyo kwa mmiliki wa jengo. 10. Mratibu wa Huduma za Mtaa. Jiji la Iowa lina mratibu wa huduma za mtaa. Ili upate taarifa zaidi, piga simu kwa 319-356-5237 au utembelee www.icgov.org/neighborhoodservices. 11. Sheria ya Jimbo. Sheria ya Ujumla ya Makazi ya Mpangishaji na Mpangaji ya Iowa (Sheria ya Iowa Sura ya 562A) inaweza kupatikana kwenye Maktaba ya Umma ya Jiji la Iowa na inaweza pia kupatikana kwenye www.legis.iowa.gov. 12. Malipo ya awali ya Kodi. Sheria ya Iowa juu ya malipo ya awali ya kodi inaweza kupatikana kwenye Sehemu ya 562A.12 ya Sheria ya Iowa. Mpangishaji ana haki ya kushikilia malipo ya awali ya kodi (pia yanajulikana kama dhamana ya kodi) kiasi hicho kama kinachokubalika na muhimu kurejesha makazi katika hali ya awali ya mwanzo wa upangaji, isipokuwa uchakavu wa kawaida. Wapangaji wanatakiwa kumpa mpangishaji anwani ya barua au maelekezo ya uwasilishaji kwa mpangishaji kwa ajili ya urejeshwaji wa malipo ya awali ya kodi. Taarifa zaidi zinazohusiana na upangaji, kuingia,kutoka, na mahitaji vinaweza kupatikana kwenye https://offcampushousing.uiowa.edu/resource/iowa?p=tenant. 13. Maeneo ya Mafuriko. Ramani ya maeneo ya mafuriko inapatikana kuonyesha iwapo nyumba hii iko katika maeneo ya mafuriko. Ili upate ramani, nenda kwenye http://bit.ly/2CTwFnE_FloodplainRentals. Sisi, tunaosaini, tumesoma fomu ya Utambuzi na Ufumbuzi wa Taarifa na kukamilisha kujaza maeneo yaliyo wazi kwa ufahamu wangu mzuri. Mpangishaji: ______________________________ Tarehe: ______________________________________ Mpangaji: _________________________________ Tarehe: ______________________________________ Mpangaji: _________________________________ Tarehe: ______________________________________ Mpangaji: _________________________________ Tarehe: ______________________________________ Mpangaji: _________________________________ Tarehe: ______________________________________ Mpangaji: _________________________________ Tarehe: ______________________________________ **Kumbuka** Wapangaji wote, isipokuwa watoto wadogo wa wapangaji, wanapaswa kusaini fomu hii hata kama wana makubaliano ya matamshi ya upangaji.