HomeMy WebLinkAboutBLM Resolution 6-16-20 SwahiliNAMBARI YA UAMUZI. ____20-159_____
Uamuzi wa Ahadi za Kwanza za Baraza zinazoshughulikia Vuguvugu la
Maisha ya Watu Weusi ni Muhimu na Ubaguzi wa Rangi wa Kimfumo
kufuatia kuuawa kwa George Floyd na Polisi wa Minneapolis na miito ya
kuchukua hatua kutoka kwa wenyeji na waandamaji.
Kwa kuzingatia kuwa maandamano yametanda kote nchini na Iowa City kutokana na kuuawa
kwa George Floyd na polisi wa Minneapolis; na
Kwa kuzingatia kuwa Jiji la Iowa City linaunga mkono kwa dhati haki muhimu ya kikatiba ya haki
ya kujieleza na kukusanyika, jinsi inavyotekelezwa katika maandamano ya amani; na
Kwa kuzingatia kuwa wenyeji na waandamaji wanasisitiza kuwa Jiji na Baraza la Jiji lichukue
hatua ili kushughulikia vuguvugu la Maisha ya Watu Weusi ni Muhimu na Ubaguzi wa Rangi wa
Kimfumo; na
Kwa kuzingatia kuwa ubaguzi wa rangi wa kimfumo umekithiri zaidi katika mfumo wa nchi na jiji
letu hivi kwamba juhudi pana na za kina zitahitajika; na
Kwa kuzingatia kuwa Baraza la Jiji limejitolea kutekeleza juhudi hizo na ni kwa ajili ya masilahi
bora zaidi ya Jiji la Iowa City na wakazi wake; na
Kwa kuzingatia kuwa Baraza la Jiji lingependa kuanza kutekeleza ahadi zake za kwanza kwa
vuguvugu la Maisha ya Watu Weusi ni Muhimu.
Kwa hivyo, sasa, Baraza la Jiji la Jiji la Iowa City, Iowa, limeamua kuwa:
Baraza linaahidi kutekeleza juhudi pana na za kina ili kushughulikia vuguvugu la Maisha ya
Watu Weusi ni Muhimu na ubaguzi wa rangi wa kimfumo, ikiwa ni pamoja na yafuatayo:
1. Kubuni mpango wa mwanzo wa kuweka mpangilio mpya wa Idara ya Polisi ya Iowa City
(ICPD) ili kufanya polisi wafahamikiane na wenyeji, ikiwa ni pamoja na kupunguza hali
ya umma kutegemea zaidi polisi katika hali zisizo za vurugu kupitia kutumia wataalamu
ambao hawajajihami na kuzingatia mipango ya polisi kufahamikiana na wenyeji katika
miji mingine, ikiwa ni pamoja na Minneapolis, MN, Camden, NJ, Los Angeles, CA na
San Francisco, CA kufikia tarehe 15 Desemba 2020; na
2. Kutenga fedha za Jiji za kiasi cha $1,000,000 wakati wa Mwaka wa Bajeti kuanzia
tarehe 1 Julai 2020 kwa juhudi za kuendeleza usawa wa rangi na haki ya kijamii, ikiwa ni
pamoja na kupanua mpango wa Ushirikishaji wa Watu Maalum [SPI], kubuni mpango
mpya mkubwa wa nyumba za bei nafuu, ikiwa ni pamoja na kujenga nyumba mjini na
mitaa ya karibu, kuunga mkono juhudi zinazotarajiwa kubainishwa za Tume ya Ukweli
na Upatanishi na kufanya kipindi cha kazi ya Baraza mnamo au kabla ya tarehe 1 Agosti
2020 ili kushughulikia utengaji mahususi; na,
Nambari ya Uamuzi. ___20-159____
Ukurasa wa 2
3. Kuendeleza juhudi za Jiji za usawa wa rangi na haki ya kijamii, ikiwa ni pamoja na
kupanua juhudi za kuongeza idadi ya walio wachache wanaoajiriwa na Jiji ikiwa ni
pamoja na kuondoa vizuizi vya kutuma maombi ya kazi, kuongeza nyenzo zilizotengwa
kwa ajili ya juhudi hizo jinsi inavyohitajika ili kuwapa mafunzo wafanyakazi wote wa jiji
kwa njia bora na kuratibu na kuripoti kuhusu matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya
usawa wa rangi na haki ya kijamii; na,
4. Kufikia tarehe 1 Agosti 2020, kupokea ripoti kutoka kwa Msimamizi wa Jiji kuhusu
kushiriki kwa ICDP katika matumizi ya gesi na magruneti ya kutoa mwangaza mwingi
wakati wa maandamano Iowa City tarehe 3 Juni 2020; na,
5. Kufikia tarehe 1 Oktoba 2020, kubuni Tume ya Ukweli na Upatanishi ili kutoa ushahidi
kuhusu ukweli wa kutokuwepo kwa usawa wa rangi Iowa City na kutekeleza haki ya
urejesho, kupitia ukusanyaji wa ushahidi na maoni ya umma na kazi kama hiyo
ijumuishe mapendekezo kwa Baraza kuhusu mpango wa kutenga na/au kubadilisha
majina ya maeneo ya umma na/au haki za njia ya kuheshimu vuguvugu la Maisha ya
Watu Weusi ni Muhimu; na,
6. Kufanya kiwe kipaumbele cha 2021 cha sheria ya Baraza la Jiji ya kutetea na kuunga
mkono ujumbe wetu wa jimbo katika kutekeleza mageuzi ya haki za uhalifu, kuondoa
vita dhidi ya dawa za kulevya na kufanya mabadiliko kwenye sheria ya jimbo ambayo
inawezesha mpango wa Jiji wa kuweka mpangilio mpya wa idara ya polisi, kuimarisha
mamlaka ya Bodi ya Jamii ya Ukaguzi wa Polisi (CPRB) na kupunguza tabia zisizofaa
za walio wachache, ikiwa ni pamoja na kuunga mkono sheria ya jimbo ya kutochukua
sheria za kihalifu dhidi ya kiasi kidogo cha bangi; na,
7. Kuendelea kutumia zana za usawa wa rangi na idara za jiji na kuendeleza mafunzo
kama hayo kwa Baraza la Jiji na kushirikiana na washirika wetu wa biashara za eneo ili
kuelimisha na kufunza wanabiashara kuhusu kutumia zana za usawa wa rangi; na,
8. Kuomba na kupokea ripoti na mapendekezo kutoka kwa CPRB kufikia tarehe 1 Januari
2021, kwa kushauriana na mwanasheria itakayomchagua, kuhusiana na mabadiliko
kwenye sheria ya CPRB ambayo inaimarisha uwezo wake wa kutoa maarifa kwa umma
kuhusu ICPD, ikiwa ni pamoja na yale yanayoshughulikia ushahidi wa kushawishi wa
polisi na ripoti ijumuishe muhtasari wa mbinu zinazokubalika na zinazokataliwa na
CPRB, iwe ni kwa ajili sababu za kisheria au za sera; na,
9. Kuelekeza wafanyakazi kutoa muhtasari wa kina wa matumizi ya fedha za bajeti ya
polisi kwenye tovuti ya Jiji; na,
10. Kutuma barua iliyoambatishwa kama Ushahidi wa “A” kwa Liwali wa Kaunti ya Johnson
inayounga mkono kuacha kutumika kwa gari la MRAP (Mine Resistant Ambush
Protected) na kupata ripoti kutoka kwa wafanyakazi wa jiji kuhusu silaha za kiwango cha
kijeshi zilizo katika orodha ya ICPD na mikataba ya nchi ambayo inatoa usaidizi kwa
idara ya polisi; na,
Nambari ya Uamuzi. ___20-159____
Ukurasa wa 3
11. Kumwelekeza Msimamizi wa Jiji kupiga marufuku moja kwa moja matumizi yoyote ya
kumbana mtu shingo au njia nyingine yoyote ambayo inasimamisha mzunguko wa damu
au kuingia kwa hewa mwilini katika sheria za jumla za ICPD; na,
12. Kumwelekeza Msimamizi wa Jiji kuhakikisha kuwa desturi na sera za ICPD
zinazohusiana na kuajiri polisi zinalingana na malengo yaliyotolewa hivi majuzi ya Iowa
House File 2647 ili kuhakikisha kuwa poilisi wanaofanya kazi Iowa hawajatekeleza kosa
lolote kubwa, jinsi inavyobainishwa.; na,
13. Kumwelekeza Msimamizi wa Jiji kukagua mifumo na mbinu za kuripoti zinazotumika
katika ICPD ili kutathmini iwapo zinatii sheria za ICPD za Kamera Zinazovaliwa Mwilini
na sheria ya jumla ya Rekoda za Ndani ya Gari, kuhakikisha kuwa mifumo kama hiyo
inatii kikamilifu sheria ya jumla, kuikagua jinsi inavyohitajika ili kutimiza lengo hilo,
kujumuisha athari kamili za kutotii sheria na kuripoti kwa Baraza baada ya kukamilisha
ukaguzi.; na,
14. Kumwelekeza Msimamizi wa Jiji kukagua sheria za jumla za ICPD ili kuhitaji polisi
waingilie kati na kukomesha matumizi ya nguvu kupita kiasi ya polisi wengine na kuripoti
tukio moja kwa moja kwa msimamizi na kuweka makubaliano ya uelewano na mashirika
mengine ya eneo ya kutekeleza sheria kuhusu uingiliaji kati kama huo wakati nguvu
kupita kiasi inatumika na polisi wa shirika lingine kama ile ambayo inajadiliwa kwa sasa
na kusambazwa miongoni mwa mashirika ya eneo ya kutekeleza sheria iliyoambatishwa
kama Ushahidi wa “B”; na,
15. Kuomba na kupokea na mapendekezo kutoka kwa Kamati ya Jiji ya Ushauri wa Sanaa
ya Umma, baada ya kupokea maoni na kushauriana na wasanii Weusi wa eneo kuhusu
mbinu ambazo Tume inapaswa kuzingatia ili kutoa fursa kwa maonyesho ya kisanaa na
vuguvugu la Maisha ya Watu Weusi ni Muhimu na jamii za watu weupe, ikiwa ni pamoja
na sanaa za kuona pamoja na tamasha la umma lililotengwa kwa ajili ya kusherehekea
utamaduni wa Watu Weusi.
16. Kupiga marufuku matumizi ya vitoa machozi, risasi bandia na magruneti ya kutoa
mwangaza mkali dhidi ya maandamano ya amani.
17. Kuanzia mwaka wa 2021, sherehe za maadhimisho ya ukombozi wa watumwa nchini
Marekani, tarehe 19 Juni, itakuwa sikukuu ya jiji na itachukua nafasi ya sherehe ya jiji
iliyopo.
Umepitishwa na kuidhinishwa siku hii ya tarehe 16 Juni 2020.
________________________________________
Meya
Umeidhinishwa na:
Shahidi: ___________________________ ______________________________
Karani wa Jiji Ofisi ya Mwanasheria wa Jiji (17/06/2020)
Nambari ya Uamuzi. ___20-159____
Ukurasa wa 2
Ulipendekezwa na __________________ na kuungwa mkono na ________________ Uamuzi
uanze kutumika na baada ya kuita orodha ya majina ya waliopo, kulikuwa na:
Wanaounga Mkono: Wanaopinga: Ambao Hawakuhudhuria:
__X____ ______ _______ Bergus
__X____ ______ _______ Mims
__X_____ ______ _______ Salih
__X____ ______ _______ Taylor
__X____ ______ _______ Teague
__X___ ______ _______ Thomas
__X____ ______ _______ Weiner
USHAHIDI WA A
Tarehe 17 Juni 2020
Lonny Pulkrabek
Liwali wa Kaunti ya Johnson
S.L.P 2540
511 S. Capitol Street
Iowa City, IA 52244
Mpendwa Liwali Pulkrabek,
Kwa niaba ya Baraza la Jiji la Iowa City, ninaandika ili kuomba kuwa ofisi ya Liwali iache kutumia gari la
MRAP (Mine-Resistant Ambush Protected). Gari la kiwango cha kijeshi lililobuniwa kutumika katika
maeneo ya vita halifai kutumika na shirika la eneo la kutekeleza sheria. Hali hii inadunisha imani ya
umma kwa mashirika ya utekelezaji wa sheria na hivyo basi kuathiri lengo la kudumisha usalama wa
jamii
Asante kwa kuelewa.
Wako mwaminifu,
Bruce Teague, Meya
Jiji la Iowa City
JIJI LA IOWA CITY
410 East Washington Street
Iowa City, Iowa 55240-1826
(319) 356-5000
(319) 356-5009 FAKSI
www.icgov.org
USHAHIDI WA B
MAKUBALIANO YA UELEWANO
Tarehe: Juni 10 2020
MAKUBALIANO haya ya UELEWANO yamewekwa kati ya Idara ya Liwali ya Kaunti ya Johnson,
Idara ya Polisi ya Iowa City, Idara ya Usalama wa Umma ya Chuo Kikuu cha Iowa, Idara ya Polisi ya
Coralville, Idara ya Polisi ya North Liberty na Idara ya Polisi ya University Heights ili kuwapa mamlaka
polisi wetu wa kutekeleza sheria kutoka katika kila mojawapo ya eneo la mamlaka kuingilia kati iwapo
watashuhudia matumizi ya nguvu kupita kiasi.
WAJIBU WA KUINGILIA KATI
Polisi yeyote wa kutekeleza sheria anayeshuhudia polisi mwingine wa kutekeleza sheria akitumia nguvu
kupita kiasi ambayo haifai kutumika kulingana na hali iliyopo atakuwa na uwezo iwapo anaweza kufanya
hivyo, kusihi ili kuzuia matumizi ya nguvu kupita kiasi.
Polisi na manaibu wao walioapishwa wanapaswa kulinda umma na wafanyakazi wengine bila kujali kazi,
cheo au shirika la mwanachama na wanapaswa kuingilia kati kimwili na kwa maneno kwa njia salama.
Polisi wa kutekeleza sheria anayeshuhudia mfanyakazi mwingine akitumia nguvu kupita kiasi kuliko jinsi
inavyoruhusiwa kisheria anapaswa kuripoti haraka iwezekanavyo hali hii kwa msimamizi.
Tunakubali na kuwajibu kwa jamii tunazohudumia.
Ni mimi wako,
Bill Campbell, Mkuu wa Polisi wa Iowa City Scott Beckner, Mkurugenzi wa Usalama wa Umma
wa Chuo Kikuu cha lowa
Lonny Pulkrabek, Liwali wa Kaunti ya
Johnson
Diane Venenga, Mkuu wa Polisi wa North
Liberty
Shane Kron, Mkuu wa Polisi wa Coralville
Troy Kelsay, Mkuu wa Polisi wa University Heights
Tarehe 17 Juni 2020
Janet Lyness
Mwanasheria wa Kaunti ya Johnson
417 S. Clinton Street
Iowa City, IA 52240
Mpendwa mwanasheria wa Kaunti Lyness,
Kwa niaba ya Baraza la Jiji na kwa mujibu wa mjadala uliopitishwa na Baraza la Jiji katika Mkutano wake
Maalum wa Baraza mnamo tarehe 16 Juni 2020 ili kujadili Maisha ya Wetu Weusi ni Muhimu/Ubaguzi wa
Rangi wa Kimfumo/Sera za Polisi, ninaomba kuwa kesi zote unazoshughulikia dhidi ya waandamaji wa
Maisha ya Watu Weusi ni Muhimu zifutiliwe mbali.
Nimeambatisha muhtasari uliotolewa kwa Baraza na idara ya polisi wa maandamano na kesi zinazohusiana
na trafiki zilizowasilishwa na ICPD kati ya tarehe 30/05/2020 na tarehe 09/6/2020 zinazokaribiana na
maeneo ya maandamano, tarehe na saa.
Asante kwa kuelewa.
Wako mwaminifu,
Bruce Teague, Meya
Jiji la Iowa City
Viambatisho.
JIJI LA IOWA CITY
410 East Washington Street
Iowa City, Iowa 55240-1826
(319) 356-5000
(319) 356-5009 FAKSI
www.icgov.org
Tarehe/Saa
(24HRS) Eneo Jiji la Makazi ya
Mshitakiwa MAKOSA Ushahidi
wa Polisi
KUTIWA
MBARONI
ALIKAMATWA
KISHERIA?
20200530
1:55
S CAPITOL ST/
COURT ST
GARNER, IA KUENDESHA GARI
UKIWA
UMEKUNYWA
POMBE AU
KUTUMIA DAWA
NYINGINE -
INASUBIRI
MATOKEO
HAPANA inasubiri
matokeo
HAPANA
20200530
23:17
E BURLINGTON
ST/JOHNSON ST
NORTH
LIBERTY, IA
KUENDESHA GARI
KWA KASI YA JUU
NDIYO HAPANA HAPANA
20200605
21:45
E BURLINGTON
ST/S SUMMIT ST
IOWA CITY, IA KUENDESHA GARI
UKIWA UMEPIGWA
MARUFUKU
HAPANA NDIYO HAPANA
20200606
19:46
E COLLEGE ST/
S VAN BUREN ST
MOUNT
PLEASANT, IA
ISHARA YA
KUSIMAMA
NDIYO HAPANA HAPANA
20200606
20:30
HWY 1 W/MILLER
AVE
IOWA CITY, IA KASI NDIYO HAPANA HAPANA
20200607
00:55
410 E
WASHINGTON
ST
CEDAR
RAPIDS, IA
KUENDESHA GARI
UKIWA
UMEKUNYWA
POMBE AU
KUTUMIA DAWA
NYINGINE, PCS
BANGI, KUMILIKI
BUNDUKI UKIWA
UMEKUNYWA
POMBE AU
KUTUMIA DAWA
NYINGINE
NDIYO NDIYO HAPANA
20200607
1:31
S GILBERT ST/
E COLLEGE ST
IOWA CITY, IA KUKIUKA IDHINI YA
MAAGIZO,
KUSHINDWA
KUTOA
UTHIBITISHO WA
DHIMA YA
KIFEDHA
NDIYO HAPANA NDIYO
20200607
01:33
HWY 1 W/
ORCHARD ST
IOWA CITY, IA NAMBARI YA
USAJILI WA GARI
NDIYO HAPANA HAPANA
20200608
18:55
E BURLINGTON
ST/S DUBUQUE
ST
IOWA CITY, IA HAKUNA LESENI
YA DEREVA,
KUSHINDWA
KUTOA
UTHIBITISHO WA
DHIMA YA
KIFEDHA,
KUSHINDWA
KUONYESHA
NAMBARI YA
USAJILI WA GARI,
KUTOTUMIA
NDIYO HAPANA NDIYO
VIZURI MIKONDO
YA BARABARA
20200608
19:51
E MARKET
ST/LINN ST
IOWA CITY, IA NAMBARI YA
USAJILI WA GARI
AMBAYO MUDA
WAKE WA
KUTUMIKA
UMEKWISHA
NDIYO HAPANA HAPANA
20200609
00:09
200 S CLINTON
ST
IOWA CITY, IA KUENDESHA GARI
UKIWA
UMEKUNYWA
POMBE AU
KUTUMIA DAWA
NYINGINE
HAPANA NDIYO HAPANA
20200609
00:47
E COURT ST/
S GILBERT ST
WHEATON, IL KUMILIKI VIFAA
VYA DAWA ZA
KULEVYA
HAPANA NDIYO-
imethibitish
wa na
kutolewa
HAPANA
20200609
00:47
E COURT ST/
S GILBERT ST
IOWA CITY, IA KUMILIKI
KITAMBULISHO
KISICHO CHA
KWELI, KUMILIKI
VIFAA VYA DAWA
ZA KULEVYA
HAPANA NDIYO-
imethibitish
wa na
kutolewa
HAPANA
20200603
22:45
DUBUQUE/
FOSTER
IOWA CITY, IA TABIA ISIYOFAA,
MKUTANO WA
KINYUME CHA
SHERIA
HAPANA NDIYO HAPANA
20200603
23:45
DUBUQUE/
MEADOW RIDGE
LANE
IOWA CITY, IA MKUTANO WA
KINYUME CHA
SHERIA, KUKATAA
KUTAWANYIKA
HAPANA NDIYO HAPANA